Dodoma FM

Waziri Dkt. Gwajima amshukuru Rais Samia kuimulika sekta ya maendeleo ya jamii

2 April 2021, 10:38 am

Na; Mariam Matundu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dorothy Gwajima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza nguvu katika Wizara hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa Sekta ya maendeleo ya jamii.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akimkaribisha Naibu Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Mwanaidi Ali Khamis.

Amesema kuwa Maendeleo ya Jamii ni  kitovu cha maendeleo ya Taifa na kama Sekta za maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii zikisimamiwa vizuri, sekta zingine nitapata ufanisi na hivyo kuharakisha Maendeleo kwa Taifa zima.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamaii Dkt. John Jingu amemuhakikishia Naibu Waziri huyo kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha matokea na matarajio ya  Rais  yanafanikiwa.

Akizungumza mara baada ya kukaribishwa Wizarani Naibu Waziri huyo anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema kuwa atafanya kazi kwa ustadi na kwa kasi ili kuhakikisha kuwa sekta anazosimamia zinakuwa na maendeleo na kutoa matokeo chanya na yanayo nufaisha  jamii.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Mhe. Mwanaidi Ali Khamis aliteuliwa na Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan Machi 31, 2021 na kuapishwa April 1, 2021 kushika nafasi hiyo na kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa Naibu Waziri wa Fedha