Dodoma FM

Mila na desturi kiini cha ukatili kwa jamii.

2 April 2021, 8:55 am

Na; Alfred Bulahya.

Wajumbe wa kamati za ulinzi wa mwanamke na mtoto (MTAKUWA) waliopo wilayani Chamwino  Jijini Dodoma, wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kuibua vitendo vya ukatili na kupeleka kesi hizo kwenye mamalaka husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi utakaosaidia kukomesha vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa miradi kutoka shirika la Women Wake Up (WOWAP) wakati akizungumza baada ya kikao na wajumbe hao kilichofanyika wilayani humo  ambacho kili wakuwakutanisha wajumbe wa ngazi ya kata na vijiji.

Amesema lengo la kukutana na wajumbe hao ni kuhakikisha wanarekebisha mapungufu yanayokwamisha jitihada za kukomesha vitendo hivyo na ametoa wito kwa halmashauri kuzisimamia kamati hizo ili zitekeleze majukumu yake ipasavyo.

Nae Afisa ustawi kutoka halmashauri ya wilaya ya Chamwino bw. Lucas kaombwe, amesema wameamua kuwaita wajumbe hao ambao ni wenyeviti na watendaji wa kata na vijiji wakiamini wao ndio wasimamizi wakubwa wa masauala hayo kwenye maeneo yao.

Amesema uelewa mdogo wa jamii nyingi dhidi ya ukatili ni moja ya sababu zinazo changia vitendo vya kikatili kuendelea huku mila na desturi zikichangia kwa kiasi kikubwa.

Ester Paul na Benedictor Thomas, ni baadhi ya watendaji walioshiriki kikao hicho kutoka kijiji cha Mahama na Nzali, wamesema wamejifunza namna watakavyo kwenda kukabiliana na suala hilo kwani ukatili dhidi ya wanawake na watoto unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa hofu na kukwamisha ndoto za wanawake wengi.