Dodoma FM

Wabunge wateule wala kiapo bungeni

1 April 2021, 7:48 am

Na; Mariam Kasawa

Spika wa Bunge Job Ndugai amewaapisha wabunge watatu wa kuteuliwa na Rais leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 bungeni mjini Dodoma.

Walioapishwa ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi Bashiru Ally na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana Jumatano Machi 31, 2021.

Wateule hao walishangiliwa na wabunge wengine wakati wakiingia katika ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria kwa ajiliya kuapa.