Dodoma FM

Maboresho yachangia ongezeko la mahudhurio ya kliniki kwa wajawazito

30 March 2021, 1:03 pm

Na; Mariam Matundu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema Wizara ya Afya imeboresha huduma za afya ya uzazi nchini katika kipindi Cha Julai 2020 Hadi Februari 2021 ambapo jumla ya wajawazito 1,165,526 sawa na asilimia 103 ya waliotarajiwa  walihudhuria kliniki na kupata huduma.

Dkt Gwajima amesema kuwa Kati ya wajawazito hao asilimia 36.5  walianza huduma kabla ya wiki 12 ikilinganishwa na asilimia 36.4 kipindi Kama hiki mwaka 2019.

Ameongeza kuwa asilimia 90.4 wamehudhuria mara nne au zaidi ikilinganishwa na asilimia 84.1 mwaka 2019.

Kwa upande wa waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya Dkt. Gwajima amesema wajawazito 920,126 sawa na asilimia 82 Kama ilivyokua katika kipindi Kama hicho mwaka 2019.