Dodoma FM

Idilo , Mpwapwa walia na ukosefu wa huduma ya Afya

29 March 2021, 11:19 am

Na,Mindi Joseph

Wakazi wa kijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa wapo mbioni kuepukana na adha ya kukosa huduma ya Afya kijijini hapo kutokana na ujenzi wa kituo cha Afya kukaribia kukamilika.

Akizungumza na Dodoma Fm Diwani wa kata ya Mazae Mwl. William Madanya, amebainisha kuwa kata ya mazae ina zahanati moja huku kijiji cha idilo kikiwa hakina zahanati na kijiji cha kisokwe kipo katika hatua ya kupaua kituo chao na tayari serikali imetoa shilingi million 2 na laki 7 kukamilisha ujenzi huo.

Ameongeza kuwa serikal imetoa mabati 100 ili kuanza  mara moja ujenzi wa nyumba ya mganga wa hospitali ya kisokwe.

Aidha kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya kisokwe kutaongeza juhudi Zaidi kwa wananchi wa kijiji cha Idilo  kuharakisha  ujenzi wa kituo cha afya  kijiji  hapo  ambao unatarajia kuanza mwezi June mwaka huu.

Kijiji cha Idilo mpaka sasa hakina zahanati hali inachangia wananchi hao kufuata huduma ya afya kata ya Mazae Wilayani Mpwapwa.