Dodoma FM

Uwajibikaji wa Vijana ni matunda ya kumuenzi Rais Magufuli

26 March 2021, 8:13 am

Na; Selemani Kodima

Vijana Nchini wametakiwa kuendelea kuwajibika na kuonesha Uzalendo katika Majukumu yao ili kuenzi uzalendo ambao uliooneshwa na Hayati Rais Magufuli wakati wa Utawala wake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi   Mtendaji wa  Taasisi ya maendeleo ya Vijana Dodoma DOYODO Rajabu Juma,alipokuwa akizungumza na Dodoma Fm ambapo amesema Hayati  Rais Magufuli amewajali vijana kwa kuwapa nafasi za kutosha kwenye nyadhifa mbalimbali za Uongozi .

Amesema ipo haja vijana wakaendelea kudumisha Uzalendo ambao ulikuwa ni kivutio Tosha kwa Hayari Rais Magufuli katika uwajibikaji na Uongozi wake.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma Billy Chidabwa amesema watamuenzi Hayati Dkt.Magufuli kwa kuendeleza Uwazi na Uadilifu katika Nafasi watakazogombea katika Chaguzi mbalimbali katika kuwatumikia wananchi.

Pamoja hayo wamesema kuwa  wanajivunia Kitendo cha Hayati Dkt.Magufuli kuhamishia Makao Makuu ya Nchi Dodoma kwa Vitendo na kufanya Mkoa wa Dodoma kukua kiuchumi .