Dodoma FM

Tanzania itamkumbuka daima Dkt. Magufuli kuwa shujaa na mkombozi

22 March 2021, 12:50 pm

Na; Mariam Kasawa

Viongozi mbalimbali walio hudhuria katika tukio la kumuaga Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wamemzungumzia  kuwa alikuwa  shujaa na  mkombozi  waTanzania, Afrika na Duniani.

Wakizungumza katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Marais Walio hudhuria shughuli hiyo wamesema watamkumbuka Magufuli kwa ukarimu , ushauri na maoni aliyokuwa akiwapatia kipindi cha uhai wake.

Aidha wamezungumzia Magufuli kama mtu mwenye upendo ,  mzalendo wa Nchi yake na ni Rais aliyependa zaidi kukaa Nchini kwake kuliko kwenda Nchi za nje ili kuisaidia Nchi yake kutatua mambo mbalimbali.

 Wamesema kifo cha Rais Magufuli kimeacha alama kubwa katika Taifa la Tanzania pamoja na Afrika kutokana na mambo mengi aliyo yafanya  ikiwemo kuzindua miradi mbalimbali pamoja na ushirikiano na mataifa ya Afrika.

Historia aliyo itengeneza Dkt. Magufuli Tanzania na Afrika itakumbukwa Daima kwa kuyaendeleza yale yote aliyo yaacha ,  Mwenyezi Mungu amjaalie pumziko la milele.

Nae Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amewatoa wasiwasi wale wote wenye mashaka na uongozi wake .

Mama Samia amemzungumzia Dkt. John Pombe Magufuli kuwa alikuwa mlezi, mcha Mungu licha ya kuwa na taswira ya ukali, alikuwa mkweli asie ficha maovu lakini pia alikuwa mzalendo.