Dodoma FM

Kikwete asema Tanzania ipo salama mikononi mwa Rais Samia

22 March 2021, 5:24 am

Na; Mariam Kasawa

Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh.Jakaya Kikwete amesema Taifa la Tanzania lipo salama chini ya uongozi wa Rais mpya Samia Suluhu, kwani rais huyo anafahamu kile kilicho fanyika Tanzania, kinachostahili kufanyika  pamoja na mipango ya Serikali  ya miaka  mitano ijayo.

Akiandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitta, Mh. Kikwete amesema Magufuli alitakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoanza,ila kwa bahati mbaya amefariki  wakati Taifa linamuhitaji hivyo amewataka Watanzania kushirikiana na Rais Samia Suluhu .

Amesema ana imani na Rais  Samia Suluhu  Hassan kwani amekuwa makomo wa rais Tangu mwaka 2015, walipochukuwa serikali kupitia  chama cha  Mapinduzi CCM.

Kikwete amesema kuwa Taifa litamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoyafanya, akimtaja hayati Magufuli kuwa, jasiri, mzalendo na mwenye mipango aliyotekeleza.