Dodoma FM

Ratiba ya kumuaga Hayati Dr, John Pombe Magufuli Mkoani Dodoma

20 March 2021, 3:13 pm

Na; Rabiamen Shoo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Binilith Mahenge amesema Mkoa wa  Dodoma umepewa heshima ya kumuaga Hayati Dr. John Pombe  Magufuli kutokana na mengi aliyo yafanya katika mkoa huu ikiwemo kuhamishia makao makuu mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii wakati akitoa ratiba ya kumuaga Hayati Dr John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kuandaa shughuli ya maombolezo ya na kumuaga Rais Magufuli kutoka na nafasi aliyo upa mkoa wa Dodoma pamoja na kuwa mkazi wa kudumu katika Ikulu ya Chamwini.

Amesema Hayati Dr. John Pombe Magufuli alifadhili utekelezaji wa miradi muhimu ya kimkakati ya miundombinu iliyo pamba jiji la Dodoma na kuupa  hadhi Mkoa huu kuwa Makao makuu ya Nchi mkakati ulio Dumu kwa zaidi ya miongo minne bila kutekelezwa.

Aidha amewakaribisha wakazi wote wa Dodoma pamoja na Mikoa mingine kuja kushiriki shughuli hii ya kumuaga Hayati rais Dr. John Pombe Magufuli amesema shughuli za kusaini kitabu cha maomboleza zimeanza leo  20 Machi katika viwanja vya mwalim  Nyerere mjini Dodoma hivyo wananchi wameombwa kushiriki kwa wingi kusaini kitabu hicho.

Amesema mwili wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli utawasili Mjini Dodoma jumapili katika uwanja wa ndege mjini Dodoma machi 21 saa kumi jioni na kuelekea katika ikulu iliyopo Chamwino.

Amesema baada ya kuwasili mwili huo utapitishwa sehemu zifuatazo barabara ya Chako ni chako na baadae barabara ya Nyerere, Raund abaut kwa Mkuu wa Mkoa ,  Bunge, barabara ya Morena na Buigiri hivyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kujipanga pembezoni mwa barabara ili kutoa heshima zao za mwisho.

Mkuu wa mkoa amesema  tarehe 22 Machi 2021  mwili wa Hayati  Dr John Pombe Magufuli utatokea Ikuli  Chamwino na kupitia barabara mpya ya Mfugale na kupitia Buigiri , Morena , Bunge na Barabara ya Nyerere wakati ukiwasiri viwanja vya Jamuhuri mjini Dodoma ambapo zoezi la kutoa heshima za mwisho litaanza saa kumi na mbili asubuhi na litaendelea hadi wananchi watakapo malizika.

Katika zoezi hilo kutakuwa na gwaride maalum kutoka katika jeshi la wananchi wa Tanzania, dua na sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini pamoja na Salam mbalimbali kutoka kwa viongozi.

Akihitimisha Ratiba hiyo mkuu wa mkoa amesema mwili  wa Hayati Dr. John Magufuli  utaondoka kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa  siku ya jumanne 23  Machi  kupitia maeneo yafuatayo  barabara ya UDOM, Morena, Bunge, Raund about, Chako ni chako .

Shughuli hizo zitaambatana na zoezi la  kumkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Samia Suluhu Hasana  katika Mkoa huu wa Dodoma .