Dodoma FM

Watanzania waaswa kuendelea kuliombea Taifa

18 March 2021, 9:50 am

Na, Mariam Kasawa.

Askofu Dkt.Fredrick Shoo akiteta jambo na rais Dkt.John Magufuli wakati wa uhai wake

Watanzania  wametakiwa kuendelea kumuomba Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu  ili kuliwezesha Taifa kusonga mbele.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo leo wakati akitoa salamu za pole kuhusiana na kifo cha kiongozi huyo, kilichotokea jana Machi 17, 2021.

Amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  na kuwaomba Watanzania kuendelea kuwa na umoja.

Pia ametoa  pole kwa Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu, familia ya Rais Magufuli, na Watanzania wote kwa ujumla.