Dodoma FM

Wakazi wa Dodoma wayakumbuka mema ya Magufuli

18 March 2021, 12:59 pm

Na , Yusuph Hans,

Moja ya Alama Kuu aliyoiacha Rais wa Awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli hususan kwa wakazi wa  Mkoa wa Dodoma ni pamoja na kuhamishia shughuli zote za Kiserikali Mkoani hapa.

Wakizungumza na Taswira ya habari Wananchi hao wamesema wanajivunia Tunu nyingi kutoka kwa Rais Magufuli, moja wapo ikiwa  ni Ndoto ya Rais wa Awamu ya kwanza Mwalimu Julius Nyerere kuhamishia Serikali Mkoani  Dodoma ambapo Rais Magufuli aliifanya kwa ufanisi.

Wameongeza kuwa kuhamishia Serikali Mkoani Dodoma kuliibua fursa nyingi za Maendeleo ikiwemo Biashara, Uwekezaji pamoja na uboreshaji wa Miundombinu.

Nao baadhi ya Wajasiriamali wameeleza namna Rais Magufuli alivyo wasaidia Wafanyabiashara wadogo wadogo kunufaika na Vitambulisho vya Ujasiriamali ambavyo vimewawezesha kufanya shughuli zao kwa Uhuru.