Dodoma FM

REPOA:Vijana elfu 60 wapata ajira kwenye sekta rasmi

16 March 2021, 9:31 am

Na,Mindi Joseph, Dodoma.

Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya vijana elfu hamsini hadi elfu sitini ni miongoni mwa vijana milioni moja wanaoingia kwenye soko la ajira, na kubahatika kupata ajira kwenye sekta rasmi kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Utafiti Sera na Uchumi REPOA.

Taswira ya habari imezungumza na mkurungezi wa tafiti za kimkakati kutoka taasisi hiyo Bw.Jamal Msami, ambaye amesema utafiti uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2018 na kukamilika mwaka 2019 umebaini bado kuna changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa REPOA, Dkt. Donald Mmari amebainisha kuwa wanaendela kuangalia namna ya kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za uzalishaji zinazoendana na soko la sasa, ikiwa ni pamoja na kuzindua vitabu viwili vinavyolenga kutoa maarifa zaidi.

Aidha utafiti uliofanywa nchini mwaka 2013 na Shirika la kazi Duniani ILO unaonyesha kuwa, vijana hutumia wastani wa miezi 19.4 kutafuta ajira sawa na wastani wa miezi 21 bila ajira.