Dodoma FM

Wananchi Makulu wachekelea umeme wa REA

5 March 2021, 1:14 pm

Na,Victor Chigwada,

Dodoma.

Wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma wameishukuru Serikali kwa kufanikisha kusambaza umeme kupitia mpango wa umeme Vijijini REA, kwani kwa sasa huduma hiyo imefikia idadi kubwa ya kaya.

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wanachi hao wamesema kuwa changamoto iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu ya umeme kwa kiasi kikubwa huku wakisubiri awamu ya tatu kwa maeneo yaliyobaki.

Naye Bw.Leonard Ndama ambaye ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Msangalale Magharibi amekiri kuwa baadhi ya maeneo hayajafikiwa na nishati hiyo, huku akithibitisha zoezi la utekekelezaji kwa hatua ya upimaji wa nguzo tayari limeshafanyika.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Bw.Fadhili Chibago amesema kuwa changamoto ya umeme katika Kata yake siyo kubwa kama ilivyokuwa awali, na tayari awamu ya tatu ya utekelezaji imeanza kushughulikiwa kwenye maeneo mbalimbali katika Kata yake ikiwa ni pamoja na Njedengwa.