Dodoma FM

RALEIGH:Vijana tumieni mitandao kuhamasisha utunzaji wa mazingira

19 February 2021, 2:58 pm

Na, Benard Filbert,

Dodoma.

Vijana wameshauriwa kutumia teknolojia ya uwepo wa mitandao ya kijamii katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na taswira ya habari afisa mazingira kutoka jumuiya ya vijana RALEIGH ambayo inajihusisha na utunzaji wa mazingira nchini Bw.Elibariki Saimon Mpanda, amesema vijana wanatakiwa kutumia teknolojia vizuri ili iwasaidie katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira.

Amesema changamoto kubwa hivi sasa vijana wengi hawapendi kutumia mitandao ya kijamii katika kufanya vitu vyenye matokeo chanya badala yake wamekuwa wakiitumia kufuatilia vitu ambavyo havina manufaa kwao.

Baadhi ya vijana wakizungumza na taswira ya habari wamekiri kuwa hawatumii mitandao ya kijamii katika suala la utunzaji wa mazingira kutokana na wengi wao kuwa na fikra potofu.

Juimuiya ya vijana Tanzania RALEIGH imekuwa ikijihusisha kuelimisha jamii kutunza mazingira kupitia mitandao ya kijamii ili kupata idadi kubwa ya vijana inayosaidia jamii.