Dodoma FM

Wananchi Makanda walia na ubovu wa barabara

17 February 2021, 6:28 am

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Moja ya barabara zilizoharibiwa na mafuriko

Wakazi wa kata ya makanda Wilayani Manyoni wameiomba serikali kufanya ukarabati wa barabara ya Makanda –Kintiku iliyopeteza mawasiliano tangu mwezi desemba mwaka jana 2020.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema kuharibika kwa barabara hiyo kumesababisha bidhaa kupanda mara dufu na wakinamama wajawazito wanapata taabu wanapotaka kwenda kujifungua .
Taswiara ya habari imemtafuta diwani wa Kata ya Makanda Bw.Jumanne Shaaba Mlagaza ambapo amesema tayari amewasiliana na mbunge wa jimbo hilo pamoja na TARURA ili kutatua changamoto hiyo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu .
Hata hivyo meneja wa TARURA Wilaya ya Manyoni Mhandisi Yose Mushi amesema mwaka huu barabara hiyo ipo katika mpango wa matengenezo na tayari mkandarasi ameshapatikana lakini wanasubiri mvua kupungua ili kuanza ukarabati huo .
Aidha amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara hiyo kwani wamekuwa wakichangia kuharibika kwa barabara hiyo kutokana na shughuli za kibinamu .
Barabara ya Makanda –Kintiku yenye urefu wa takribani kilometa 31 imekuwa ikileta changamoto kila wakati wa mvua za masika na kusababisha adha kwa wakazi wa maeneo hayo.