Dodoma FM

Viongozi wa dini watakiwa kukemea ukatili kwa vitendo

11 February 2021, 1:34 pm

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Wito umetolewa kwa viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuelekeza jamii mambo mema, ikiwepo kupinga na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Hayo yameelezwa na shekhe Abdishakul Maulid wakati akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kinachorushwa hapa Dodoma Fm, ambapo amesema viongozi wa dini ndio kimbilio la jamii kwakuwa wao wanaaminika, hivyo ni lazima kutumia uaminifu huo kutenda mema na si kuwa miongoni mwa wanaoshiriki kufanya ukatili wa kijinsia .

Nae afisa ustawi wa jamii jiji la Dodoma Rebeka Ndaki, amewataka wazazi na walezi kuwachunguza watoto wao ili kujua kama wanafanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na kutambua viashiria vya mtoto aliefanyiwa ukatili, ili kuripoti katika vyombo vya sheria.

Akitolea ufafanuzi suala la elimu ya afya ya uzazi daktari kutoka UMATI Elisha Makarabo amesema wameanzisha huduma za afya ya uzazi kwa vijana pekee kila mwishoni mwa wiki, ambapo pia hutolewa elimu mbalimbali.