Dodoma FM

Wizara yakabidhi mikataba minne kwa wakandarasi

2 February 2021, 1:37 pm

Waziri wa mawasiliano na teknolojia Dkt.Faustine Ndugulile wa pili kushoto

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari hii leo imekabidhi mikataba minne kwa wakandarasi wa ujenzi , upanuzi na uunganishaji wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano na miundombinu ya anwari za makazi na postikodi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Faustine Ndugulile, amesema hadi sasa mkongo wa Taifa umefanikiwa kujenga kilomita 7,910 ambapo mikataba iliyosainiwa leo inakwenda kuongeza kilomita 409 zilizolenga kufikia maeneo ya kimkakati.

Amesema lengo la serikali ni kurahisisha mawasiliano baina yake na wananchi , kuwezesha kufanyika biashara mtandao pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na madeni ya mikopo kwa urahisi kwakuwa anwari zitawezesha wadaiwa kutambulika wanapoishi.

Kwa niaba ya kampuni zilizopewa mikataba ,Mkurugenzi wa kampuni ya Radi Faiba Ramadhani Mlanzi ameishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa.

Wiraza imetoa mikataba 4 kwa kampunzi za wazalendo za RADI FAIBA,TTCL na TANZU yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.5,kwa kampuni,