Dodoma FM

Kambi za kitaaluma zachochea ufaulu Bahi

20 January 2021, 1:23 pm

Na,Seleman Kodima,

Dodoma.

Uwepo wa kambi katika shule za msingi kwa madarasa ya Mitihani katika Kata ya Bahi Wilayani Bahi imetajwa kama sababu ya Ongezeko la Ufaulu wa Darasa la saba kwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Diwani wa kata hiyo Augustino Ndunu wakati akielezea mkakati wa Kata yake katika kuhakikisha Ongezeko la Ufaulu wa darasa la saba unaongezeka mara dufu .
Amesema hivi karibuni wamekuwa na utaratibu wa kuwa na kambi za masomo kwa shule za msingi ikiwa ni mpango ambao wazazi waliafiki na kuwa sehemu ya kuchangia gharama zote kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani.

Aidha amesema baada ya Ongezeko la ufaulu wa wanafunzi ambao wanatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza imesababisha Uongozi wa Wilaya na Kata ya Bahi kuanza Ujenzi wa madarasa mawili ya sekondari ya Nagulo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi hao.