Dodoma FM

TAKUKURU Dodoma yaanza na taasisi na mashirika 2021

18 January 2021, 1:40 pm

Na,Mindi Joseph,                                

Dodoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Dodoma imesema katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 kuanzia January hadi machi itaweka mkazo katika  kuchunguza ubadhilifu wa fedha za umma na taasisi binafisi.

Akizungumza na Taswira ya habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma sosthens Kibwengo amebainisha kuwa katika katika uchunguzi walioufanya walipokea malalamiko 178 kwa mwaka 2020 na serikali za mitaa zikiongoza kwa asilimia 23.

Baadhi ya wananchi wamebainisha kuwa Tanzania ipo katika uchumi wa kati hivyo jamii inawajibu wa kutengeneza kizazi endelevu kitakachopinga Rushwa.