Dodoma FM

CVT yatoa huduma ya uchunguzi wa macho bure

18 January 2021, 1:28 pm

Na,Alfred Bulahya,

Dodoma.

Hospitali ya macho ya CVT iliyopo Uzunguni jijini Dodoma imeanza kampeni ya uchunguzi na kupima macho bure kuanzia leo Januari 28 mwaka huu, kwa lengo la kuwawezesha watu wenye vipato vya chini kupata huduma hiyo.
Akizungumza na taswira ya habari ofisini kwake meneja wa hospitali hiyo Lulu Molel amesema kuwa kampeni hiyo itawezesha watu kufanya vipimo vya macho na uchunguzi bure ambapo watu watakaobainika kuwa na tatizo lolote watapatiwa huduma za miwani na upasuaji kwa gharama nafuu.

Dkt Iyan Novatus Macha ni mmoja wa matabibu katika hospitali hiyo amesema kwa siku ya leo wamebaini uwepo wa wagonjwa wengi wanaosumbuliwa tatizo la uoni hafifu wa karibu huku matatizo mengine yakiwa ni uoni hafifu wa mbali, mtoto wa jicho, pamoja na mboni kuwa na vidonda au mkwaruzo.