Dodoma FM

Meya:Wekeni utaratibu kwa wajasiriamali kufanya shughuli zao

13 January 2021, 9:02 am

Dodoma.

Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Devis Mwamfupe

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imemwagiza Meneja wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma, kuweka utaratibu mzuri kwa ajili ya wajasiriamali kufanya shughuli zao kituoni hapo.
Agizo hilo limetolewa na Meya wa Jiji hilo, Profesa Davis Mwamfupe, alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kujionea hali ya huduma zinavyotolewa.
Profesa Mwamfupe amesema amebaini kuwapo mrundikano wa bidhaa katika eneo la kituo hicho, jambo ambalo linapaswa kuwekewa utaratibu.
Amemtaka meneja wa kituo kuweka utaratibu mzuri kwa ajili wajasiriamali kutokana na kufanya biashara kwenye kumbi za abiria.
Baadhi ya abiria wameomba kuandaliwe utaratibu mzuri ili kuepusha usumbufu pamoja na kulinda mali zao.