Dodoma FM

Jezi Dodoma Jiji Fc zawasili

12 January 2021, 9:39 am

Afisa habari wa Dodoma Jiji Fc Mosess Ntagazi akimkabidhi jezi mpya mtangazaji wa kipindi cha Michezo Sports Bomba Dodoma Fm 98.4 Seleman Kodima mara baada ya kutangaza kuwasili kwa jezi hizo

Dodoma.

Jezi za timu ya Dodoma Jiji Fc tayari zimewasili jijini Dodoma.Kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Klabu hiyo Fortunatus John ‘Foty” jezi hizo zilichelewa kuwasili nchini kutokana janga la Covid-19 lililotokea nchini China ambapo ndipo zilipokuwa zikitengenezwa.

“Tumeleta mzigo mkubwa,na zitauzwa kwa bei rafiki ambayo kila mtu ataimudu”,

“Jezi zitauzwa shilinge elfu 20,000 tu na ni moja ya jezi zenye ubora wa juu kabisa” alisema Foty wakati akizungumza katika kipindi cha Sports Bomba Dodoma Fm 98.4.

Katibu wa timu ya Dodoma Jiji Fc akizungumza ndani ya Kipindi cha Sports Bomba Dodoma Fm hapo jana,pembeni yake ni Meneja Usajili wa timu hiyo Jeremiah “Chiddo”

Kwa mujibu wa katibu huyo jezi zinapatikana katika duka la vifaa vya michezo Isere Sports lililopo maeneo ya Mji Mpya karibu na Mambo Poa na pia kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji (Majengo ya Zamani CDA).