Dodoma FM

Baobab Queens ni wa moto kweli kweli

12 January 2021, 8:16 am

Dodoma

Timu ya Baobab Queens ya Dodoma imeibuka na ushindi wa bao 6-1 dhidi ya TSC Queens ya Mwanza katika mechi ya ligi kuu soka ya Wanawake iliyopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 timu hiyo ilionesha soka safi lililowavutia mashabiki waliokuwepo uwanjani.Mabao ya Baobab Queens yamefungwa na Jamila Rajab ‘Doxa” aliyefunga manne huku mabao mengine yakifungwa na Martha John na Rehema John.Akizungumza na Sports Bomba ya 98.4 Dodoma Fm afisa habari wa timu hiyo Timothy Franciss amesema kikosi kimeanza safari kurejea jijini Dodoma kwa ajili ya kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Alliance Girls itakayopigwa katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma.Michezo mingine ya ligi hiyo Yanga Princess wameifunga Mapinduzi Queens 7-0,Es Unyanyembe wamekubali kipigo cha bao 16-1 dhidi ya Simba Queens,JKT Queens wameibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ruvuma Queens huku Alliance Girls wakiwanyamazisha Tanzanite Queens 3-2.