Dodoma FM

Wananchi Chilonwa waomba kukarabatiwa daraja

5 January 2021, 3:21 pm

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Wakazi wa kijiji cha Mahama Kata ya Chilonwa Wilayani Chamwino wameiomba Serikali kufanya ukarabati wa daraja lililopo kati ya kijiji cha mahama na Nzali ili kuondoa adha ya usafiri wanayokutana nayo kipindi cha mvua za masika.
Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya wakati hao wamesema wanashindwa kusafiri na kupata huduma mbalimbali kutokana na daraja hilo kujaa maji hali inayosababisha mabasi kushindwa kuvuka eneo hilo kutokana na miundombinu ya daraja kuwa hatarishi kwa kuwa hakuna kiashiria kinachoonesha mwanzo na mwisho wa daraja.Asheri zephania Mkosi ni mwenyekiti wa kijiji cha Mahama amesema kwa mwaka huu 2021 tayari daraja hilo limesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watano kuokolewa wakati wakijaribu kuvuka eneo hilo na kukosea njia kutokana na kukosekana kwa kingo za daraja.
Nae Diwani wa Kata ya Chilonwa Hausa Mtuza amesema tayari wamewasiliana na Mbunge wa Chamwino mh.Deo ndejembi ambae amefanya mawasilano na Tanroad na makubaliano ya awali ni kuweka mabomba ya kuonesha mwanzo na mwishowa daraja.