Dodoma FM

Afisa kilimo:Acheni kukaa ofisini

14 December 2020, 2:40 pm

Na Thadey Tesha,

Dodoma.

Wadau wa kilimo nchini wameshauriwa kuwa na mazoea ya kuwatembelea wakulima mara kwa mara kwa lengo la kuwapa elimu ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa chakula nchini.
Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa Mkoa wa Dodoma Bw.Benard Abraham ambae pia ni mshauri wa kilimo wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amebainisha kuwa kupungua kwa eneo la uzalishaji kunatokana na idadi ya watu kuongezeka pamoja na kukosa elimu ya namna ya kuongeza thamani ya mazao.

Aidha ametoa wito kwa wakulima mkoani Dodoma kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo mtama pamoja na uwele kutokana na Mkoa huo kuwa na mvua za wastani ya mili lita 400 hadi 600 pamoja na kuweka makinga maji ya mvua.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya kilimo ambae pia ni afisa kilimo wa jiji la Dodoma Bi.Yustina Munishi amesema wakulima pia wanayo fursa ya kuchukua mikopo kwa ajili ya kilimo jambo litakalowasaidia kuzalisha chakula cha kutosha.
Nao baadhi ya wadau kilimo Mkoani Dodoma wameahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa kuwatembelea wakulima ili waweze kuongeza kasi ya uzalishaji wa chakula nchini.