Dodoma FM

Baloteli ajiunga na Monza ya daraja la pili Italia

8 December 2020, 7:55 am

Mario Baloteli miaka ya nyuma akiwa Manchester City

Monza, Italia.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia, Mario Balotelli ambaye amekuwa bila klabu tangu majira ya joto, Sasa anarejea Katika Soka akijiunga na klabu cha daraja la pili huko Italia AC Monza inayomilikiwa na Silvio Berlusconi na Adriano Galliani.

Klabu hiyo inamilikiwa na Silvio Berlusconi na Adriano Galliani.
Balotelli mwenye umri wa miaka 30 ambaye amecheza Katika Vilabu vikubwa Ulaya kama Milan, Man City, Liverpool na Nice miaka ya nyuma, amefanyiwa vipimo vya afya jana Jumatatu na kusaini Mkataba ambao utamfanya abaki na Monza hadi Juni 2021.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia , Mario Balotelli ambaye amekuwa bila klabu tangu msimu wa majira ya joto, Sasa anarejea Katika Soka katika daraja la pili huko Italia ndani ya AC Monza.

Katika Klabu hiyo atakutana na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana, Kevin Prince Boateng ambaye anakipiga hapo.