Dodoma FM

Africa CDC:Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona yakaribia milioni 2.25

7 December 2020, 12:51 pm

Adis Ababa,

Ethiopia.

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimesema hadi kufikia Jumapili alasiri, idadi ya jumla ya maambukizi yaliyothibitishwa ya virusi vya Corona barani humo imekaribia milioni 2.25, huku idadi ya vifo ikifikia 53,543.

Kwa mujibu wa Africa CDC, nchi za Afrika zilizoathiriwa vibaya zaidi na virusi hivyo ni Afrika Kusini, Morocco, Misri na Ethiopia.