Chai FM

Bei ya ndizi kushuka kilio kwa wakulima

12 September 2022, 5:26 pm

RUNGWE-MBEYA,

NA:LOVENESS RAJABU

Wafanyabiashara wa ndizi wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameeleza bei ya ndizi kwa kipindi hiki cha kiangazi.
Wakizungumza na Chai FM wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Mabonde wamesema kuwa kwa sasa bei ya ndizi ipo chini ukilinganisha na bei ya zamani hivyo wanapata hasara kwani wao wananunua ndizi kwa bei ya chini lakini wanauza kwa bei ya chini.

Kwa upande wao wanunuzi wa ndizi katika soko hilo wamesema kuwa bei ya ndizi ipo juu kulingana na hali ya hewa hivyo wao kama wanunuzi wanapata changamoto katika manunuzi ya ndizi hizo kulingana na bei elekezi ya wauzaji.

Nae Daniel Jackson Mwakobela Mwenyekiti wa wafanyabishara wilayani Rungwe amesema kuwa bei ya ndizi inatofautiana kulingana na ukomavu na ukubwa wa ndizi inapelekea bei kupanda na kupungua ambapo kwa mkungu uliokaa unauzwa kwa shilingi 20 na kwa mkungu ambao haujakomaa unauzwa kaw shilingi elfu 8.

Aidha amesema kuwa wao kama wafanyabiashara wanaendana na bei kulingana na hali iliyopo huku akiongeza kuwa kushuka kwa bei ya ndizi kunasaidia kuleta unafuu kwa wananchi hasa kwa kipindi hiki ambacho bidhaa nyingi zimepanda bei.