wakulima elfu 17 tayari wamesajiliwa Mbolea ya ruzuku
9 September 2022, 9:51 am
RUNGWE-MBEYA
NA:LETHISIA SHIMBI
Wakulima wilayani rungwe Mkoani mbeya wametakiwa kufuata taratibu wa kujisajili kwenye mfumo Ili kuweza kupata Ruzuku za pembejeo.
Akizungumza na kituo Chai FM afisa kilimo wilayani hapa JUMA MZARA amesema katika halmashauri ya Rungwe wamesajiri wakulima elfu 17 kupitia mfumo na wamepata namba ya usajili.
Aidha ameendelea kwa kusema kuwa wakulima ambao hawajapata namba kutokana na changamoto za kimfumo wataenda kuwapatia namba pindi mfumbo utakapofanikiwa kukamilisha taarifa zao.
Pia MZARA amesema kuna mawakala kadhaa ambao waliomba vibali vya kusambaza pembejeo tayari washaanza kufanya kazi ya kugawa mbolea za Ruzuku kwa wakulima na kwa mfumo wa mwaka huu mkulima wa kijijini anatakiwa kwenda kununua mbolea ya ruzuku kwenye maduka ya pembejeo ya mawakala.