kilio uhaba wa maji Rungwe kupata tiba mwezi oktoba
9 September 2022, 10:15 am
RUNGWE-MBEYA
NA:WANDE BUSHU
Wananchi wa Kitongoji cha Kawetele chini Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya huduma ya maji iliyo dumu kwa muda mrefu licha la kulipia bili ya maji kila mwezi
Wakizungumza na Chai Fm wamesema kuwa hali ya kukosekana kwa maji katika kitongoji hicho kunaweza kuleta athari kama vile mlipuko wa magonjwa yanatokana na uchafu wa mazingira kutokana na kukosekana kwa Maji.
Tusubhilege Mwasoni na William Banda ambao ni wakazi wa Mtaa huo wamewaomba Viongozi husika kuwasaidia kuepukana na adha ya maji wanayokumbana nayo kwani imewalazimu kutembea umbali mrefu kufata huduma hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji Alphonce Mwabhulondo amesema amezungumza na viongozi wa mamlaka bila kupewa ushirikiano wowote hivyo anaendelea kuiomba idara husika kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Tukuyu mjini Bw Peter Amon amesema kufikia tarehe 30 mwezi wa kumi mwaka huu wananchi watapata maji kwa utoshelevu kwani maboresho ya miundombinu ya maji inaendelea kufanyiwa marekebisho.