Jamii itoe taarifa kuhusu vitendo vya ukatili
9 September 2022, 9:57 am
RUNGWE-MBEYA.
NA:LETHISIA SHIMBI
Baadhi ya Wanawake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameeleza namna wanavyoshiriki kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.
Wakizungumza na chai fm BAHATI SIMON na MAIDASI NDAMU wamesema endapo vitendo vya kikatili vikajitokeza kwenye jamii wapo tayari kutoa ushirikiano na kumsaidia mhusika kufika eneo husika kupata msaada wa kisheria.
Kwa upande wao wananchi wilayani Rungwe wamesema vitendo vya kikatili vimekithiri kwenye jamii hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutoa taarifa za vitendo vya kikatili bila kusita kuanzia ngazi ya kijiji hadi Wilaya ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.
Naye Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto na makundi maalum DKT.DOROTHY GWAJIMA amesema Serikali inaendelea kupambana na vitendo vya ukatili na kuwataka wananchi kuendelea kufichua vitendo hivyo.