Chai FM

Mradi wa pamoja wa Wakulima wa Chai Rungwe na Busokelo wafanya uchaguzi wa wajumbe wa bodi

22 May 2022, 5:57 am

RUNGWE-MBEYA.
NA:EZEKIEL KAPONELA
Mradi wa pamoja wa Wakulima wa Chai Rungwe na Busokelo (RBTC-JE) Tarehe 20.5. 2022 kimefanya uchaguzi wa wajumbe wa bodi, mwenyekiti na makamu mwenyekiti baada ya uongozi uliokuwa madarakani kumaliza muda wake wa miaka mitatu tangu walipochaguliwa mwaka 2019
Awali kabla ya kuvunjwa kwa bodi hiyo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya mradi wa pamoja Rungwe na Busokelo Ndg. Andrew Mwandemanie amewashukuru wajumbe na wanachama wote kwa namna walivyoshirikiana naye kwa kipindi chote alichoKuwa madarakani.


Kwa upande wake Bw Issa Mwanyumba ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti amewataka wajumbe na wanachama wote wa RBTC-JE kushirikiana katika kutekeleza majukumu huku wakitanguliza upendo na ushirikiano ili kufikia malengo kwa wakulima wa Chai.
Katika uchaguzi mwenyekiti aliyekuwa madarakani amepata kura 11 na aliyekuwa makamu wake katika kipindi kilichopita amepata kura 13.ambapo wajumbe 24 wameshiriki uchaguzi huo chini ya usimamizi kutoka ofisi ya ushirika Dodoma ikiwakilishwa na Bi Grace Mwangende na ofisi ya Mrajisi Mbeya chini ya Mrajisi msaidizi mkoa Ndg Richard Zengo.
Aidha msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Salence Mwakanyamale kuwa makamu mwenyekiti baada ya wajumbe wa mkutano kupiga kura kati ya wagombea 3 ameshinda kwa kura 11 kati ya kura 24 zilizopigwa.