Chai FM

Jamii itoe taarifa vitendo vya ukatili kwenye madawati

3 April 2022, 6:24 am

RUNGWE-MBEYA

Taasisi isiyo ya kiserikali inayotekeleza mradi wa mwanamke imara WiLDAF imetaka jamii kutoa taarifa kwenye madawati ya kijinsia pindi vitendo vya ukatili vinapojitokeza katika jamii.

kauli hiyo imetolewa wana Mwanasheria  SUZAN KAWANGA  pamoja na mwelimishaji  Ndg THOMAS  MPONDA  waliopokuwa wakitoa elimu kwa njia ya radio Chai FM huku wakisema kuwa jamii inapaswa kuwa karibu na watoto  katika malezi ili kuweza kupata taarifa kwa watoto

Kwa upande wake thomas mponda alianza kwa kuelezea maana ya ukatili na ukatili wa kijinsia

kwa upande mwingine THOMAS MPONDA  amewaomba wanaume kutoa taarifa kwenye vyombo na madawati pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na kutaka jamii kuacha vitende vya ukatili.

hata hivyo Mwanasheria  SUZAN KAWANGA ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwenye vyombo vinavyo sikiliza kesi kwani kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kushindwa kutoa ushirikiano na kesi kumalizwa kienyeji.