Chai FM

Jicho la mama mkombozi wa watoto yatima na wasiojiweza Rungwe

16 March 2022, 11:11 am

RUNGWE,

Na Sabina Martin

Msaada wa mahitaji mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi laki sita umetolewa kwa watoto yatima katika kituo cha kulelea watoto hao cha Igongwe wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha jicho la Mama kutokea KK Bi. Irene Sila Ngogo amesema kwamba Msaada huo umetolewa kwa kundi hilo la watoto yatima kutokana na uhitaji mkubwa walionao watoto hao ukilinganisha na makundi mengine katika jamii.

Bi Irene amesema kikundi cha Jicho la Mama kinatarajia kutoa elimu kwa jamii kwa lengo la kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la watoto wa mitaani, kwa kuelimisha zaidi juu ya malezi bora ya watoto kwa lengo la kujiepusha na akundi mabaya katika jami.

Mwalimu Kotas Mbwilo ni mtaalamu wa saikolojia ametoa rai kwa jamii kuiweka wazi migogoro katika familia zao kwa lengo la kuimarisha furaha ya familia kwa ustawi wa malezi bora ya watoto wao.

Baadhi ya wajumbe wa kikundi ch a jicho la mama wakikabidhi msaada katika kituo cha kulelea watoto yatima Igogwe

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa kikundi hicho cha Jicho la mama wametoa rai kwa jamii kuwa na utaratibu wa kuwatembelea makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii, huku wakitoa taswira ya kikundi chao namna kinavyoisaidia jamii inayowazunguka.

Kikundi cha Jicho la mama chenye makao yake eneo la KK kilianzishwa mwaka jana wa 2021 kikiwa na lengo la kusaidia wanawake na makundi mengine yenye uhitaji katika jamii ambacho kwa mwaka huu kimeadhimisha siku ya mwanamke mwishoni mwa juma kwa kutoa misaada mbalimbali.