Chai FM

Uhaba wa soko kilio wakulima wa ndizi Rungwe

14 February 2022, 12:45 pm

RUNGWE-MBEYA

Kukosekana kwa soko la uhakika la ndizi imetajwa kuwa sababu inayopelekea wakulima wa zao hilo kuuza mazao yao kabla ya wakati husika.

Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wakulima wilayani Rungwe  ambapo wamesema kuwa inawalazimu kuuza ndizi zao mashambani  kabla ya muda wake kufika na hali ngumu ya maisha imekuwa ni sababu.

Bi.STELA ISSA na SUZANA AIZAK wamesema kuwa kutokana na hali  hiyo inawaathiri wakulima kwani wanauza kwa bei ya hasara ambapo wanufaika wakubwa  ni  wafanyabiashara pindi zao hilo linapofikia muda wake kupelekwa sokoni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa gulio la Ndizi Mabonde Ndg.AMANI AMBENDWILE amewataka  wakulima wa zao hilo kuwa wavumilivu na kuachana na tabia ya kuuza ndizi zikiwa bado kufikia muda wake hali inayowanyonya wakulima katika zao la ndizi.