Chai FM

UWT Rungwe wapanda miti 50 kuendeleza uhifadhi wa Mazingira

1 February 2022, 5:22 am

RUNGWE-MBEYA

Jumla ya miti hamsini imepandwa na Umoja wa wanawake  wa chama cha mapinduzi CCM(UWT) wilayani  Rungwe mkoani Mbeya katika Zahanati ya Suma pamoja na ofisi ya chama kwenye kata hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanziswa kwa chama hicho na kuitaka jamii kuhifadhi mazingira.

Katika maadhisho hayo Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja ya wanawake BI.TWITIKE MWALWAMA amesema wamepanda miti hiyo ndani ya kata ya Suma ikiwa ni ishara ya kuienzi kazi inayofanyika na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh, Samia Suluhu Hassan katika kazi aliyo ifanya ndani ya kata hiyo ya Suma na wilaya ya Rungwe kwa ujumla.

Kwa upande wake Mgeni rasmi  kwenye hafla hiyo ambaye ni Mwenyekit wa chama cha mapindunzi wila ya Rungwe Ndg. SAM MWAKAPALA amesema wananchi pamoja na wanachama wanakila sababu ya kukienzi chama cha mapinduzi kutokana na historia nzuri ya chama kwani tangu kuazishwa kwake kimewatumikia wananchi kwa kiwango kikubwa ikiwa kuwaeletea maendeleo katika sekta mbalimbali.

Hata hiyo Mwakapala ametumia nafasi hiyo kuwa kumbusha wanachama na watanzania kwa ujumla kuwa mwaka huu ni mwaka wa sensa na makazi hiyo wanachi watoe ushirikiano katika kuhesabiwa kwani lengo la serikali ni kujua idadi ya watu wake ili iweze kuwatumikia kwa kuwapelekea maendeleo kwa idadi husika

Aidha mwakapala ameendelea kuwaomba wanachi kutowafisha watu wenye mahitji maalumu ndani ili wasiweze kuhesabiwa kwani mtu mlemvu ni haki yake kuesabiwa kwa lengo la kupatiwa haki zake za msingi ikiwemo mikopo inayo tolewa na serikali