Chai FM

Madarasa 24 yakamilikika kwa asilimia 100

3 January 2022, 9:46 am

RUNGWE-MBEYA

Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Busokelo Bi, LOEMA PETER  amekabidhi takribani vyumba vya madarasa 24 kwa Mkuu wa wilaya ya Rungwe  baada ya kumalika ndani ya muda ulio pangwa.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na kituo hiki huku akieleza kuwa  makabidhiano  yamefanyika december 30 mwaka 2021  na kusema vyumba hivyo vimekamilika kwa asilimia mia moja  na kila chumba kikiwa na madawati kwa maandalizi ya muhula  wa masomo januari 2022.

Hata hivyo Bi LOEMA  amesema  kutokana na fedha hizo za ujenzi wa vyumba vya madarasa,kama halmashauri ya Busokeko katika  ujenzi huo wamejenga ofisi za walimu ili kuwaondolea adha walimu ya kutumia chumba kimoja.

Aidha amewaomba wazazi na walezi kuwaandalia watoto sare za shule pamoja na kutoa fedha ya chakula  ili wawanafunzi wawezi kusoma bila usumbufu na kuendelea kuongeza ufaulu katika shule zilizomo ndani ya halmashauri.

sanjari na hilo Mkurugenzi huyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh, SAMIA SULUHU HASAN kwa kumuondolea mwananchi usumbufu wa kuchangia ujenzi wa madarasa kwa kutoa fedha nchi mzima kwajili ya ujenzi huo wa vyumba vya madarasa.