Chai FM

Wizara ya Elimu itenge fedha kwajili ya  ukarabati wa shule kongwe nchini

28 November 2021, 8:37 am

RUNGWE-MBEYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM  MAJALIWA ameagiza wizara ya Elimu kutenga fedha kwajili ya  ukarabati wa shule zote kongwe nchini.

Maagizo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali Mkoani Mbeya wilayani Rungwe Novemba 27 mwaka huu baada ya kujionea uchakafu wa majengo kwenye shule ya sekondari ya wasichana  Kayuki

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya JUMA HOMELA akimkaribisha waziri mkuu wakati wa kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa ujenzi wa vyumba vya mabdarasa kwa wilaya ya Rungwe amesema ujenzi wa vyumba hivyo umeanza mara moja baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu na ujenzi unaendelea

Aidha Waziri Mkuu majaliwa amesema serikali inaendelea kutoa fedha kwajili ya kuboresha  sekta ya elimu kwaanzia ngazi ya  awali hadi elimu ya juu na amefurahishwa na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shuleni hapo Kayuki.

Hata hivyo majaliwa amesema serikali inampango kuzikarabati shulele zote kongwe nchini ili wanafunzi wasome vizuri bila changangamoto zozote

Sambamba na hili Waziri mkuu amempongeza mkuu washule ya wasichana Kayuki wa kusimamia vizuri suala la taaluma kwa wanafunzi na kumtaka kundelea kuwa na moyo huo mzuri wa usimamiaji .