Chai FM

Mkuu wa wilaya Rungwe amaliza mgogoro wa shule

4 November 2021, 4:46 am

RUNGWE

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dr VICENT ANNEY, ameruhusu kuendelea kwa ujenzi wa shule ya sekondari Kibisi ambao ulikuwa umeingia kwenye mvutano baada ya kiasi cha shilingi  mil 40 kilicho tengwa kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya shule kupelekwa katika shule ya sekondari Kyimo iliyopo kata ya Kyimo Wilayani Rungwe.

Dr Anney ametoa maagizo hayo kwenye mkutano na wanakijiji hao uliofanyika katika kijiji cha Kibisi na ujenzi huo uendelee kwa nguvu za wananchi kama kawaida kwani ni kweli upo umuhimu wa kujengwa kwa shule kijijini hapo hivyo endapo ujenzi huo utakamilika mapema shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi kuanzia  mwezi Januari  2022.

Kwa upande wake afisa Elimu halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mwl MWAISAKA, amewashukuru wakazi hao wa Kibisi kwa juhudi zao za kuunga shughuli za maendeleo katika sekta ya elimu na kuwaomba kuendelea kuijenga shule hiyo ili kufikia vigezo sahihi vya serikali .

BARAKA MWAKIKUTI, ni mwenyekiti kitongoji Kibisi ameshukuru ujio wa Mkuu wa wilaya katika kata yao kwani sasa yale yote waliyo agizwa kuyatekeleza yanakwenda kufanikiwa na amewaomba wananchi kushirika katika kuchangia michango pale inapohitajika na kuachana na maswala ya siasa kwani hayatasaidia kukamilika kwa ujenzi wa shule yao.

JOB MWANKAYE na DOMITINA SANGA, ni wakazi wa kitongoji cha kibisi wamesema kwa kuwaomba vijana wanao hamasisha migomo isiyo kuwa na tija ya watu kuto kuchangia michango ya ujenzi wa shule yao waache kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya kijiji.