Chai FM

Mila na desturi zinavyokandamiza wagonjwa wa akili

21 October 2021, 9:33 am

RUNGWE

Hivi karibuni Dunia imeadhimisha siku ya magonjwa ya afya ya akili jamii wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ametakiwa kuachana na imani za kishirikiana juu ya ugonjwa huo.

Akizungumza na kituo hiki mratibu wa afya ya akili wilaya Dkt JOHN DUNCAN amesema jamii imekuwa ikihusiainisha magonjwa ya afya ya akili na ushirikina bila kufika katika vituo vya afya kufanya uchunguzi na kupatiwa matibabu.

Sanjari na hayo Dkt Duncan ametaja sababu mbalimbali zinazopelekea magonjwa ya afya ya akili ikiwemo msongo wa mawazo, hitilafu katika mfumo wa ubongo, magonjwa ya kudumu na wengine kurithi kutoka kwenye familia.

Pia amesema kundi la Vijana limekuwa likiathirika zaidi na ugonjwa wa afya ya akili kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na makundi rika yamekuwa yakichanigia ongezeko ilo.
Hata hivyo ameitaka Jamii kuachana na unyanyapaa kwa wagonjwa wa afya ya akili na badala yake kuonesha upendo na kuwapatia matibabu.