UMEME WALETA MGAO WA MAJI MKOANI MBEYA

Maji ni uhai,viumbe wote hai wanategemea maji hata nje ya viumbe hai bado kumekuwa na uhitaji wa maji,nchi ya Tanzania imekuwa ikitegemea maji kuzalisha nishati ya maji hivyo kwa hali hiyo unweza kusema maji na umeme vinategemeana.

Afisa mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya Neema Stanton(Picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya(WSSA)imekri kuwepo kwa mgao wa maji chanzo kikitajwa kuwa ni upungufu wa maji kwenye vyanzo vya kuzalishia maji pamoja na kukatika katika kwa umeme.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya Neema Stantony wakati akieleza namna ambavyo mamlaka hiyo inavyofanya kazi kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na tatizo la kukatikakatika kwa umeme.

sauti ya neema stanton afisa mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya

Bi,Neema amesema kama mamlaka inafanya jitihada mbalimblai za kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa kila mwananchi sambamba na hayo afisa huyo amewashauri wananchi kuhifadhi maji kwenye vyombo pindi yanapopatikana kutokana na zamu zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Neema Stanton afisa mawasiliano na uhusiano wa WSSA Mbeya akiwa studio za Baraka Fm,akieleza umuhimu wa wananchi kuhifadhi maji kipindi hiki chenye changamoto ya upatikanaji wa maji(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya afisa mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya Neema Stanton

Nao baadhi ya watumiaji wa maji ambao ni wakazi wa jiji la Mbeya wameeleza namna ambavyo kero ya maji imekuwa ikiwaathiriambapo wamesema maji hayo yamekuwa yakitoka kwa mgao iwe kijijini au mjini.

sauti za baadhi ya wananchi wa jiji la Mbeya wakieleza namna kero ya maji inavyowakabili

sa