Baraka FM

Mbeya kuanza kutoa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka 8

15 September 2023, 22:46

Afisa chanjo jiji la mbeya Christopher Mathias akiwa amefika katika ofisi za radio Baraka Fm Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)

Wanasema kinga ni bora kuliko tiba,ili uweze kuwa salama huna budii kukubaliana na ushauri wa wataalamu wa afya unaopatiwa juu ya afya yako.kila binadamu tangu kuzaliwa kwake lazima apewe chanjo ili kuweza kuimarisha afya yake, hali hiyo ukiwa kama mzazi au mlezi unapaswa kuilinda familia yako kwa kuwapatiwa chanjo kupitia vituo vya afya vilivyokaribu nawe.

na Hobokela Lwinga

Wazazi na walezi mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza na kuwapeleka watoto wenye umri wa miaka chini miaka 8 kupata chanjo ya Polio inayotarajiwa kutolewa maeneo mbalimbali kuanzia septemba 21-24 mwaka huu.

Akizungumza na kituo hiki afisa chanjo wa jiji Mbeya katika studio za Baraka fm  Christopher mathias amesema chanjo hiyo ina umuhimu mkubwa hivyo asiwepo mwananchi wa kupuuzia

Afisa chanjo jiji la Mbeya Christopher Mathias akiwa tayari katika studio za Baraka Fm kutoa hamasa ya wananchi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya polio(picha na Hobokela Lwinga)
sauti ya afisa chanjo jiji la Mbeya Christopher Mathias akitoa wito kwa wananchi kutokupuuzia chanjo ya Polio

Bw.christopher ameongeza kuwa sababu kubwa ya kufanya kampeni hiyo ni kutokana na tanzania kupata mgonjwa katika mkoa wa rukwa .

sauti ya afisa chanjo jiji la Mbeya Christopher Mathias akizungumzia lengo la utoaji wa chanjo ya Polio

Aidha afisa chanjo huyo ametaja dalili za ugonjwa wa polio kuwa ni kupata upoozi wa ghafla kwa mtoto pamoja na mtoto kuwa ni legelege huku akisema  kila mtu anaweza kupata ugonjwa wa Polio.

picha ya afisa chanjo jiji la Mbeya Christopher Mathias akiendelea kutoa elimu ya Polio katika studio za Baraka Fm(picha na Hobokela Lwinga)
sauti ya afisa chanjo jiji la mbeya Christopher Mathias akizungumzia dalili za ugonjwa Polio

Nao baadhi ya wazazi mkoani Mbeya wamesema chanjo hiyo ni muhimu wazazi wote kuhakikisha wanatoa ushirikiano mzuri kwa watakao husika kutoa chanjo hiyo.

Mtangazaji wa Baraka Fm Mpoki Japhet akiwa tayari kufanya mahojiano na afisa chanjo jiji kuhusiana na chanjo ya Polio(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za wananchi wa jiji la Mbeya wakieleza uelewa na mapokeo ya chanjo ya polio