Baraka FM

Wananchi Mbeya washauriwa kutunza mazingira ili kuepukana na athali ya mabadiliko ya tabia ya nchi

12 September 2023, 12:39

Baadhi ya wananchi mkoa wa Mbeya wakipanda miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira(picha na mwandishi wetu)

Uharibifu wa mazingira duniani kote umekuwa na athali hasi zinazosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi,na hivi karibuni tumeshuhudia athali hizo ikiwemo upungufu wa mvua

Na Hobokela Lwinga

Wananchi mkoani mbeya wameshauriwa kuwa mabalozi wazuri wa utunzaji wa mazingira ili kulinda na kuepukana na athari ambazo zinasababishwa na hali ya uharibifu wa mazingira.

Wito Huo Umetolewa Na Mwenyekiti Wa Taasisi Inajishughulisha Na Utunzaji Wa Mazingira Ya Green Awerenes Club Davina Kanani Wakati Akizungumza Na kituo hiki katika kuelekea katika siku ya misitu duniani ambayo wanatarajia kuiadhimisha  kwa kupanda miti katika shule ya msingi pambogo iliyopo jijini mbeya.

Bi,Davina amesema kila mwananchi anapaswa kuaanza kuyatunza mazingira yanayomzunguka sambamba na kutoa elimu kuanzia ngazi ya familia.

Kwa upande wake katibu wa green  awereness club Paulo Masele wameanza kupeleka kwa wanafunzi ili kuwatengeneza wanafunzi hao kuwa mabalozi kwenye jamii inayowazunguka.

Hata Hivyo Mmoja Ya Wanachama Wa Taasisi hiyo Hadija Mkumbo amesema utunzaji wa mazingira unahitaji wa ushirikiano wa kila mwananchi kwani mazingira bora ni kichocheo cha maendeleo.

Sehemu ya muonekano wa chanzo cha maji cha mto nzovwe Mbeya (picha na mwandishi wetu)

Taasisi ya utunzaji wa mazingira ya green awerenes club inatajia kupanda miti zaidi ya 200 huku kauli mbiu ya sherehe hizo ikisema mazingira safi mazingira ya kijani.