Adhana FM

Upimaji wa UVIKO 19: Wasafiri watakiwa kutuma maombi mtandaoni ili kupunguza msongamano.

6 October 2021, 6:20 am

afisa afya uwanja wa ndege Zanzibar akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya.

Radio Adhana

WASAFIRI wanaondoka nchini wametakiwa kutuma maombi kwa njia ya mtandao  ya kipimo cha uviko 19 ili kupunguza msongamano wakati wa kusafiri na kusababisha kuchelewa kwa wasafiri.

Afisa dhamana huduma za afya uwanja wa ndege  Nassor  Hamad Said amesema hayo katika ,liyofanywa na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya ya Wizara ya afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto.

Amesema iwapo wasafiri watafanya maombi kwa njia ya mtandao itawezesha kupata majibu ya kipimo ya uviko 19  mapema kupunguza  foleni wakati wa safari  na msafiri kuondoka kwa wakati .

Aidha alifahamisha ni vyema wasafiri wakawasiliana na mashirka yao ndege mapema na wakala wao wanaosafirisha kufanya maombi yao kwa njia ya mtandao ili kupunguza foleni.

Amesema mbali ya changamoto hiyo pia wanakabiliwa na uchache wa vitendea kazi pamoja na uhaba wa wafanyakazi na kupelekea kutofanya kazi kwa ufanisi uanaotakiwa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Salim Slim  amesema changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa  Kitengo cha afya Uwanja wa ndege Zanzibar  watazifanyia kazi kwa haraka ili waweze kutoa huduma bora kwa wasafiri.

Amesema wafanyakazi wa kitengo hicho wanafanya kazi kubwa ya kuwahudumia wasafiri wanaotoka na  wanaongia nchini hivyo watahakikisha huduma zinazotolewa kwa wasafiri zinakuwa ubora wa hali ya juu.

Alifahamisha kuwa   kitengo hicho kinahitaji  kuwa na wafanyakazi wa kutosha sambamba na vitendea kazi pamoja na kuimarisha mifumo ya kutoa huduma za kupima  uviko 19 kwa wasafiri wanaotoka na wanaongia nchini.